Habari Mpya:NHIF yatakiwa kuongeza wanachama wasio waajiriwa- bofya hapa kwa habari zaidi...
Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umetakiwa kuongeza jitahada za
kuwasajili wanachama wengi wa mfuko huo ili vituo vya serikali viweze
kutoa huduma kwa wananchi wengi. Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na
Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
wakati alipotembelea kituo cha afya cha Mazwi kilichopo katika Manispaa
ya Wilaya ya Sumbawanga mwishoni.
Alisema
Mkoa wa Rukwa umefikia asilimia 27 ya wananchi wanaotumia bima ya afya
Kitaifa,hivyo waongeze kuwashawishi wananchi wengi zaidi kujiunga na
mfuko huo pamoja na mfuko wa afya ya jamii(CHF).
“nimesema
kuanzia sasa ninaanza kuwapima kwa kusajili wananchi ambao hawapo
kwenye mfumo rasmi wa ajira,ninataka vijana wengi wajiunge kwa wingi kwa
kwa kujiunga kama kikundi na kujiunga na bima inayojulikana kama
‘Kikoa” kwa kujiunga kikundi cha kuanzia watu kumi,wafikieni huko huko
walipo.
Kwa
upande wa Mfuko wa Afya ya jamii(CHF) waziri huyo hivi sasa kuna CHF
iliyoboreshwa hivyo kadi hiyo inatumika kwenye vituo vyote vya
halmashauri na si pale mwanachama alipokatia,”ni bora tuwachangishe
elfu kumi kumi za watanzania ili tuweze kufikia usajili wananchi wengi
na kupata huduma za afya bila vikwazo.
Hata
hivyo alishauri Manispaa hiyo kutengezea kadi ambayo itakua rafiki kwa
mwanachama kuweza kuiweka kwenye waleti au mahali pengine ambayo itakua
rahisi kwa kutunza na siyo kadi za hivi sasa ambayo ni mzigo kwa
mwanachama kuibeba kwani kadi hiyo ni kubwa.
Aidha,alisema
wizara yake inataka kuongeza gharama ya CHF iliyoboreshwa ya shilingi
elfu ishirini ambapo mwenye kadi hiyo ataenda kupata huduma hivyo hadi
hospitali ya mkoa.
“
tunazungumzia kila mtu apate huduma za tiba bila kikwazo,leo una
hela,kesho huna na una umwa bora tunasema utoe elfu kumi na utibiwe
ndani nya manispaa tena siyo peke yako bali na watu wako watano,alisema
waziri ummy. Hata hivyo alisema ni marufuku kwa mtu mwenye kadi ya CHF
anapoenda kwenye vituo vya huduma ya afya kuambiwa akanunue kipimo au
dawa bali wanatakiwa kupata vipimo vyote.
No comments: