Habari Mpya: OPERESHANI MAALUMU YA KUPAMBANA NA KILIMO CHA BANGI, WATANO MBARONI MVOMERO- bofya hapa kwa habari zaidi...
Mkuu
wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe (aliyeshika dumu) akimimina
mafuta ili kuchoma lundo la bangi iliyokuwa imeng’olewa Augosti 19, 2017
na kikosi kazi maalumu katika moja ya mashamba ya bangi katika
kitongoji cha Lufuna, Kijiji cha Masalawe, Kata ya Luale , Tarafa ya
Mgeta, wilaya ya Mvomero .
Na John Nditi, Globu ya Jamii - Morogoro
POLISI
mkoani Morogoro kwa kushirikiana na Maofisa wa Mamlaka ya Kuthibiti na
Kupambana na Dawa za Kulevya nchini wamefanikiwa kuteketeza mashamba ya
bangi ya ukubwa wa zaidi ya ekari 25 na kuwatia mbaroni watu watano
akiwemo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Lufuna , Asteri Telesphor (27). Watu
hao miongoni mwao ni Mwenyekiti wa Kitongoji hicho baada ya kukutwa
wakijihusisha na kilimo bangi kwa njia ya umwagiliaji kando kando ya
mto Mgeta, katika kijiji cha Masalawe, Kata ya Luale , wilayani Mvomero.
Operesheni
hiyo maalumu ya kupambana na dawa za kulevya hasa kilimo cha bangi
iliyofanyika Augosti 19, mwaka huu na kuongozwa Mwenyekiti wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama mkoa , Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen
Kebwe akiwa na Maofisa wa mamlaka ya kuthibiti na kupambana na dawa za
kulevya pamoja na viongozi wa wilaya ya Mvomero.
Viongozi
mbalimbali wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoa wa Morogoro na wilaya ya
Mvomero walioongozwa na Mkuu wa mkoa Dk Kebwe Stephen Kebwe pamoja na
askari Polisi wakiwa katika zoezi la kung’oa na kufyeka miche ya bangi
kwenye moja ya mashamba ya bangi katika kitongoji cha Lufuna , Kijiji
cha Masalawe, Kata ya Luale , Tarafa ya Mgeta, wilaya ya Mvomero .
Timu
ya Opereshani hiyo ililazimika kuacha magari eneo la kijiji cha Homboza ,
Kata Mlali na kutembea kwa miguu kwa muda wa zaidi ya saa mbili
kufika katika vitongoji vya Lufuna na Tagata vilivyopo kijiji cha
Masalawe , kata ya Luale , Tarafa ya Mgeta , wilayani Mvomero kwa ajili
ya kutekeleza mashamba hayo. Kugundulika kwa mashamba hayo ni kufuatia
Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya mkoa kupata taarifa kutoka kwa wasiri
juu ya uwepo wa uzalishaji mkubwa wa bangi eneo hilo.
Akizubngumza
katika eneo la mashamba hayo , Kamishina wa Operesheni wa Mamlaka hiyo,
Mihayo Msikhela alisema , opereshani za kutekeleza dawa za kulevya
hasa mashamba ya bangi ni endelevu kwenye maeneo mbalimbali nchini na
kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama vya mikoa husika .
“
Serikali imekataza matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi na ili
kutokomeza jambo hii opereshani za kushitumiza zitaendelea kufanyik
maeneo mbalimbali nchini na kwamba serikali haijaribiwi” alisema Mihayo.
Mkuu wa
mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( mbele ) akivuka mto Mgeta
akifuatiwa na Kamishina wa Operesheni wa Mamlaka ya Kuthibiti na
Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Mihayo Msikhela , Aug 19, 2017 ili
kushiriki na kikosi kazi maalumu kwa ajili ya kuteketeza shamba la bangi
iliyolimwa kwa njia ya kilimo cha umwagiliaji kando kando mwa mto huo ,
katika kitongoji cha Lufuna , Kijiji cha Masalawe, Kata ya Luale ,
Tarafa ya Mgeta, wilaya ya Mvomero .
Naye
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema , watu
watano walikamatwa katika opereshani hiyo akiwemo Mwenyekiti wa
Kitongoji cha Lufuna , Kijiji cha Masalawe , Kata ya Luale Tarafa ya
Mgeta , Asteri Telesphor (27) baada ya kukutwa na kiroba cha bangi
iliyoivuna kutoka shambani mwake.
No comments: