Habari Mpya: RAZA AMWAGA ZAWADI MICHEZO YA MASKULI MIKOA
Na Salum Vuai, MAELEZO
MKURUGENZI
wa kampuni ya usafiri wa anga na huduma za viwanja vya ndege Zanzibar
(ZAT) Mohammedraza Hassanali, ametoa wito kwa kampuni na taasisi
mbalimbali kuunga mkono juhudi za serikali kuimarisha michezo maskulini.
Akizungungumza
wakati wa hafla ya kukabidhi vitu mbalimbali kwa ajili ya zawadi za
washindi kwenye mashindano ya mpira wa miguu mikoa ya Unguja na Pemba
iliyofanyika nyumbani kwake Kibweni, Raza alisema ni wajibu wa kila
Mzanzibari kusaidia sekta ya michezo.
Alifahamisha
kuwa, iwapo wafanyabiashara wa Zanzibar wataunganisha nguvu kwa lengo
la kuinua michezo kuanzia ngazi ya skuli ambako ndiko kwenye msingi wa
vipaji vizuri, nchi hii itafika mbali kimichezo na kulitangaza vyema
jina la Zanzibar.
“Hii
ninchi yetu sote, tuna wajibu kusaidia juhudi za serikali, na nimpongeze
Mhe. Rais kwa kuteua Mkurugenzi makini na mwenye jitihada kuongoza
Idara ya Michezo na Utamaduni,” alieleza Raza.
Mkurugenzi
Idara ya Michezo na Utamaduni katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Amali Hassan Khairalla Tawakal, akimtambulisha Mkurugenzi Uendeshaji na
Utumishi wa wizara hiyo Omar Ali Bhai kwa Mwenyekiti wa kampuni ya ZAT
Mhe. Mohammedraza Hassanali.
Mwenyekiti
wa ZAT ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mhe. Mohammedraza
Hassanali akimkabidhi kalkuleta Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi wa
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Omar Ali Bhai kwa ajili ya washindi
wa mashindano ya mpira wa miguu kwa skuli za mikoa yote ya Unguja na
Pemba inayotarajiwa kuanza Septemba 12, 2017 katika uwanja wa Amaan Mjni
Unguja.
Mkurugenzi
Idara ya Michezo na Utamaduni Hassan Khairalla Tawakal akitoa shukurani
kwa Mhe. Raza kwa msaada alioutoa kuwazawadia washindi wa michuano ya
mpira wa miguu kwa skuli za mikoa ya Zanzibar itakayofanyika mwezi ujao
mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.
No comments: