Habari Mpya: NANI MBABE NGAO YA JAMII LEO? YANGA KUENDELEZA UBABE AU SIMBA KULIPIZA KISASI?
KUELEKEA
mtanange wa kumaliza ubishi baina ya mahasimu wawili Simb ana Yanga
huku kila upande ukijinasibu kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa Ngao ya
Jamii utakaochezwa kesho kuanzia majira ya saa 11 jioni Uwanja wa Taifa
Jijini Dar es salaam.
Ni mechi ya watani wa jadi inayozungumzwa sana midomoni mwa watu,
kila mmoja akijinasibu kumfunga mwenzake kwa idadi kubwa ya magoli na na
kuinyakua Ngao ya Jamii.
Simba ikiwa imefanya usajili mkubwa sana na wagharama,
wakiwajumuisha nyota wanne kutoka Azam Fc John Bocco, Shomari Kapombe,
Aishi Manula na Erasto Nyoni pamoja na Kiungo Mnyarwanda kutoka Yanga
aliyekipiga kwa misimu kadhaa Haruna Niyonzima.
Mbali na hao, wamemsajili golikipa wa Timu ya Taifa akitokea
Mtibwa Sugar Said Dunda na Emanuel Mseja kutoka Mbao Fc, beki wa kulia
Shomary Ally, beki wa kati kutoka Toto Africa Yusuf Mlipili, Salim
Mbonde kutoka Mtibwa na Mshambuliaji Emanuel Okwi kutoka Sc Villa ya
Nchini Uganda. Nicolaus Gyan kutoka Nchini Ghana na beki wa kushoto
kutoka Mbao Jamal Mwambeleko
Kwa upande wa Yanga, wameweza kufanya usajili kwa kuwasajili
Ibrahim Ajib kutoka Simba, Raphael Daud kutoka Mbeya City, Pius Buswita
kutoka Mbao Fc, Gadiel Michael kutoka Azam, Papii Kabamba Tshishimbi wa
Mbabane Swallows na wameweza kuwapanisha vijana wao kutoka timu B Said
Musa, Maka Edward ili kuja kuziba nafasi zilizoachwa wazi na wachezaji
walioachwa pamoja na wale waliosajiliwa na timu zingine.
Yanga
walifanikiwa kuwabakisha wachezaji muhimu kama Donald Ngoma, Thaban
Kamosoku na Amisi Tambwe waliokuwa wamemaliza mikataba ya kuitumikia
klabu hiyo ya Yanga.
No comments: