Habari Mpya: MAHUJAJI WA TANZANIA WAANZA KUWASILI SAUDI ARABIA
Na Mwandishi Maalum, Riyadh, Saudi Arabia.
Mahujaji kutoka
Tanzania wameanza kuwasili nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kutekeleza nguzo ya
tano ya dini ya kiislamu ya kuhiji Makkah inayofanywa na watu mbalimbali duniani, wakiwamo Waislamu kutoka Tanzania.
Baadhi ya mahujaji wakionekana Uwanja wa Ndege baada ya kuwasili nchini Saudi Arabia kwa ajili ya swala ya Hija.
Mahujaji kutoka Tanzania wakiwa wamewasili nchini Saudi Arabia.
Baadhi ya Waislamu wanaoendelea kuwasili nchini hapa wakionekana pichani.
Ibada ya Hijja mwaka
huu inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Agosti hadi mwanzoni mwa mwezi
Septemba, huku jumla ya mahujaji 977 kutoka Tanzania
wameshawasili katika miji ya Madina na Jeddah. Mahujaji hao waliwasili katika
viwanja vya ndege vya Madina na Jeddah na kupokelewa na maafisa wa Ubalozi wa
Tanzania.
Tanzania kwa mwaka huu inataraijiwa kupeleka mahujaji wapatao 2,700. Indonesia
ndiyo nchi inayoongoza kwa kupeleka mahujaji wengi mwaka huu inatarajiwa kuwa
na mahujaji wapatao 168,000. Mwaka huu Saudi Arabia inatarajiwa kupokea
mahujaji zaidi ya 2,000,000 kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni.
No comments: