Habari Mpya: ASILIMIA KUBWA YA WANANCHI WAISHIO VIJIJINI HAWANA ELIMU YA KUTOSHA KUHUSU HUDUMA ZA MAWASILIANO -TCRA
Mjumbe
wa Baraza na Mwenyekiti wa kamati ya Elimu na Uhamasishaji Baraza la
Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano,John Njawa akizungumza
mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar
kuhusiana na utafiti walioufanya kwa Watumiaji wa huduma za mawasiliano
hivi karibuni wakishirikiana na Chuo cha Mipango cha Dododoma.Kulia ni
Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za
Mawasiliano,Mary Shao Msuya na kushoto ni Mjumbe wa Baraza na Kamati ya
Elimu Uhamisishaji -Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za
Mawasiliano (TCRA CCC),Nyanda Shuji
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo
Mjumbe
wa Baraza na Mwenyekiti wa kamati ya Elimu na Uhamasishaji Baraza la
Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano ((TCRA CCC)),John
Njawa akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa Waandishi aaliyeuliza swali
kuhusiana na utafiti huo walioufanya,mbele ya Waandishi wa habari
(hawapo pichani) mapema leo jijini Dar.Kulia ni
Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za
Mawasiliano,Mary Shao Msuya.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za
Mawasiliano,Mary Shao Msuya pamoja na Mjumbe wa Baraza na Kamati ya
Elimu Uhamisishaji -Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za
Mawasiliano (TCRA CCC),Nyanda Shuji (kushoto),wakionesha vitabu vyenye
utafiti uliofanywa na Baraza hilo kwa Watumiaji wa Huduma za
Mawasiliano,wakishirikiana na chuo cha Mipango cha Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za
Mawasiliano,Mary Msuya alisema kuwa utafiti huo umefanywa ikiwa ni moja ya mipango ya baraza hilo kwa mwaka 2016/2017.
Katika
utafiti huo,Mary alisema kuwa utafiti huo ulifanyika katika wilaya
tano,ambazo ni Manispaa ya Dodoma (Mjini),Chamwino (vijijini),Mvomero
(vijijini),Temeke Manispaa (mjini),na Kaskazini A Unguja,Zanzibar
(vijijini),alisema na kuongeza kuwa watu walioshirikishwa kwenye huduma
hizo za mawasiliano ni 697,umri kuanzia miaka 15,huku asilimia 50.5
wakiwa wanafunzi wa elimu ya shule ya msingi.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za
Mawasiliano,Mary Shao Msuya akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar
kuhusiana na utafiti walioufanya kwa Watumiaji wa huduma za mawasiliano
hivi karibuni wakishirikiana na Chuo cha Mipango cha Dododoma.
No comments: