Habari Mpya:Kampuni ya Kansai Plascon Tanzania sasa rasmi Arusha-bofya hapa kwa habari zaidi......
Arusha:
Kampuni ya Kansai Plascon Afrika ltd. Ambayo ni kampuni tanzu ya
kampuni ya rangi ya Kansai iliyoko Japan, imehitimisha makubaliano yake
ya kununua shughuli za rangi za Sadolin nchini Tanzania na nchi nyingine
za Afrika Mashariki. Hii ilitangazwa na Deodatus Makumpa Meneja wa
Kanda ya Kaskazini, Plascon Tanzania wakati akitoa taarifa kwa vyombo
vya habari katika Hotel ya Arusha Jijini Arusha
Kampuni ya rangi ya Kansai ni kampuni ya kimataifa ambayo inaendesha shughuli zake nchini Japan, China, Mashariki ya Kati, Ulaya na Afrika. Bidhaa zake inazotoa zinajumuisha upambaji, Viwanda, rangi za kulinda na mitambo, ina vituo vya utafiti na maendeleo nchini Japan, India na Afrika Kusuni.
“Tumefurahishwa na mafanikio haya. Kupitia haya, tutaweza kutumia nembo yenye nguvu ya urithi wa Kansai, uwezo wa kimataifa wa kiufundi, na utendaji wa kuaminika, kutupatia uwezo mpya, kuweza kupata teknolojia mpya na utambuzi ambao ni muhimu zaidi katika kuendelea kukuza nembo hii,” alisema Makumpa

Akiongea
kuhusu sababu za kuinunua, Gary van der Merwe, Rais wa Kampuni ya
Plascon Afrika Mashariki alisema kwamba makubaliano haya yanadhihirisha
nia ya Kansai Plascon katika kujiendeleza zaidi duniani. “Afrika
Mashariki ni moja kati ya ukanda ambao unakuwa haraka zaidi kiuchumi
barani Afrika. Kwa ukuaji wa kasi wa daraja la kati, kuongezeka kwa
nguvu ya utumiaji na kukua kwa miji, huu ni muda muafaka wa kuingiza
sokoni bidhaa zetu mbali mbali kwaajili ya kuboresha zaidi mtindo wa
maisha yao wakati huo huo tukiwa tunaongeza kuenea kwetu duniani”.
No comments: