Habari Mpya:MAKONDA ALIONGEZEA NGUVU SHIRIKA LA UTANGAZAJI TBC- bofya hapa kwa habari zaidi....
Mkuu wa Mkoa wa Dr es salaam Paul Makonda leo ametoa msaada wa Gari aina ya Noah, Pikipiki Tatu, Computer Tano na Camera Mbili za kisasa kwa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC ili kuongeza nguvu katika kuwafikia Wananchi.
Mbali na Vifaa hivyo vya kisasa pia Makonda amefanikiwa kumpata mfadhili atakaepaka Rangi Jengo lote la TBC kuanzaia siku ya kesho ili liwe na muonekano wa kisasa.
Akizungumzia baada ya kukabidhi msaada huo MAKONDA amesema lengo nikuwawezesha wananchi ambao hawana uwezo wa kuita vyombo vya habari na kueleza matatizo yao waweze kufikiwa.
Vifaa ivyo vitatumika kuongeza nguvu kwenye kipindi cha Hadubini ambacho kimekuwa kikisaidia Wananchi wanyonge kupaza sauti zao.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa TBC Bi. MARTHA SWAI amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwapatia msaada huo huku Zaituni Mkwama ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Hadubini akielezea kuwa vifaa hivyo vitawaongezea ufanisi katika kazi yao
Hilo ndilo Gari ambalo Shirika la Utangazaji la TBC wamekabidhiwa na Mkuu wa MKoa
Hizi ni Pikipiki Tatu zilizokabidhiwa kwa TBC ikiwa ni miongoni mwa vifaa vilivyotolewa na Mkuu wa Mkoa katika shirika hilo
No comments: