Habari Mpya: SIMBA MABINGWA WA NGAO YA HISANI 2017
Rais
wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallance Karia na Makamu wake,
Michael Wambura wakiwa pamoja na Wachezaji wa Timu ya Simba baada ya
kuwakabidhi Ngao ya Jamii waliyoitwaa leo baada ya kuwashinda watani wao
wa jadi Yanga kwa changamoto ya mikwaju ya penati ya 4-3, katika mchezo
uliochezwa uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo.
Kiungo
wa Yanga Haruna Niyonzima akiwania mpira wa mshambuliaji wa Yanga
Donald ngoma katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Ngao ya Jamii unaoendelea
hivi Uwanja wa Taifa.
Kiungo
wa Yanga Rafael Daud akimruka beki wa Simba Method Mwanjali katika
mchezo wa ufunguzi wa Ligi Ngao ya Jamii unaoendelea hivi sasa Uwanja wa
Taifa
Beki
wa kati wa Yanga Kelvin Yondani na mshabuliaji wa Simba Laudit Mavugo
wakigombania mpira katika mchezo wa ufunguzi wa ligi wa Ngao ya Jamii
unaoendelea hivi sasa Uwanja wa Taifa.
Mshambuliaji
wa Yanga Donald Ngoma akimruka beki wa Simba Method Mwanjali katika
mchezo wa ufunguzi wa ligi wa Ngao ya Jamii unaoendelea sasa hivi Uwanja
wa Taifa
Golikipa Rostand Youthe akiruka juu na kudaka mpira akiwa sambamba na mshabuliaji wa Simba Emanuel Okwi.
Kiungo wa Simba Haruna Niyonzima akipiga pigo la adhabu nje ya kumi na nane
Mshambuliaji
wa Yanga Donald Ngoma akipambana na beki wa kati wa Simba Salim Mbonde
katika mchezo wa ufunguzi wa ligi Ngao ya Jamii.
No comments: